Jumanne, 19 Januari 2016
Ngeli za nomino za kiswahili
SWALI:
Kwa
kutumia mifano, ainisha ngeli za nomino za Kiswahili, kwa kigezo cha
kimofolojia. Kisha jadili upungufu wa uainishaji huo.
Fasili ya ngeli
imejadiliwa na wataalamu na wanazuoni mbalimbali, huku kila mtaalamu akiwa na
mtazamo wake juu ya dhana hii. Baadhi ya wataalamu na wanazuoni hao ni kama
hawa wafuatayo:
Mgullu (1999: 148)
anasema istilahi “ngeli” imechukuliwa kutoka lugha ya Kihaya (Tanzania). Katika
lugha ya kihaya neno “ngeli” lina maana ya aina ya kitu.
Mgullu (1999: 148)
akiinukuu Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981) anaeleza kuwa ngeli ni utaratibu wa
taaluma ya sarufi ya lugha katika kupanga aina za majina (nomimo) kama vile
ki-vi, ma, n.k.
Mgullu anaendelea
kusema kuwa fasili hii inapotosha. Tuaamini ya kuwa ngeli ni kundi la nomino za
aina moja na si ule utaratibu wa kupanga nomino katika makundi kama fasili ya
hapo juu inavyodai.
TUKI (1990) wanaeleza
kuwa ngeli za nomino ni kundi moja la majina yaliyo na upatanisho wa kisarufi
unaofanana na viambishi vya umoja na wingi vinavyofanana. Fasili hii inaonekana
ni bora lakini tatizo lake ni kuwa imeweka pamoja vigezo viwili, yaani kigezo
cha kisintaksia na kile cha kimofolojia. Kwa maoni yangu ni kuwa vigezo hivi
haviwezi kutumika pamoja kwa sababu havina uhusiano wa moja kwa moja. Wanaisimu
na wachambuzi wengi wa awali walijaribu kuvitumia vigezo vyote viwili kwa
pamoja wakati wa kuainisha ngeli za nomino za Kiswahili lakini walishindwa.
Hali hii imesababisha uainishaji wa ngeli katika lugha ya Kiswahili uonekane
kuwa wa kutatanisha.
Massamba, D.P.B na
Wenzake (2012) wanasema kauli kwamba ngeli ni mgawanyiko wa aina mbalimbali za
nomino katika mtazamo wa kisarufi katika fikra ya viashirio vya nomino katika
aina nyingine za maneno zinazoandamana nazo. Kwa maelezo mafupi tunaweza kusema
ngeli za nomino huhusu makundi ya majina; kila kundi likiwa na mabadiliko ya
aina moja ya viambishi vya umoja na wingi vyenye kuleta upatanishi wa kisarufi
wa namna moja katika vitenzi, vivumishi na viwakilishi. Kila ngeli ina
kiambishi cha nomino zake ambacho kinatawala viambishi vinavyorejea nomino hiyo
katika aina hizo nyingine ziandamanazo nayo.
Massamba na Wenzake
wanaendelea kufafanua kuwa kila lugha inayotumia utaratibu wa ngeli huwa ina
idadi fulani ya ngeli. Si rahisi kusema kwa yakini hapo zamani lugha za kibantu
zilikuwa na ngeli ngapi, lakini tunajua kwamba kwa wastani lugha nyingi zina
ngeli zisizopungua kumi na zisizozidi ishirini.
Kwa ujumla, ngeli ni
aina au namna ya kupanga au kuweka majina katika makundi yanayofanana au
yanayowiana. Majina ya Kiswahili yanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali.
Baadhi ya wanaisimu wamegawanya majina katika makundi 16 na wengine katika
makundi 9 na wengine makundi 18. Wanaisimu tofauti walioainisha ngeli za majina
ya Kiswahili wamechunguza vipengele tofauti
vya majina na kuyaanisha tofauti. Nomino za lugha fulani zinaweza
kuainishwa kwa kutumia vigezo vikuu vitatu yaani:
·
Kigezo cha kisematiki
·
Kigezo cha kimofolojia
·
Kigezo cha kisintaksia
Lakini katika muktadha
huu tutajikita katika kujadili uainishaji wa ngeli za Kiswahili kwa kutumia
kigezo cha kimofolojia. Kigezo cha kimofolojia ni kigezo kikongwe zaidi
kilichotumiwa na wanasarufi mapokeo, miongoni mwao akiwa Meinhof ambao
waliyaainisha kulingana na maumbo ya viambishi awali vya majina. Majina yote
yalikuwa na viambishi awali vinavyofanana yaliwekwa katika kundi moja na
kufanya ngeli moja kutokana na kigezo hiki kuna ngeli 18 za Kiswahili.
Uainishaji wao ni kama ifuatavyo:
|
Ngeli
|
Mfano
wa majina ya Ngeli
|
|
1-Mu-
2-Wa-
|
Mzee
– wazee
Mtoto-
watoto
|
|
3-
M-
4-
Mi-
|
Mti
– miti
Mchungwa
– michungwa
|
|
5-
Ki-
6-
Vi-
|
Kiti-
viti
Kisu-
visu
|
|
7-
Ji-
8-
Ma-
|
Jiwe-
mawe
Jicho-
macho
|
|
9-
N-
10.
|
Nguo,
nchi, njaa, nyota, ngozi, nyama
|
|
11-
U-
12-
N-
|
Uso
– nyuso
Uzi
– nyuzi
Ulimi-
ndimi
|
|
13-
U-
14-
Ma-
|
Uasi
– maasi
Ugonjwa
– magonjwa
|
|
15-
Ku-
|
Kusoma
Kucheza
Kuimba
Kuruka
|
|
16-
Pa-
|
Pahali
|
|
17-
Mu-
|
Muhali
|
|
18-
Ku-
|
Kuhali
|
Wanaisimu wengine
Ashtoni (1944) na Broomfield (1930) waliainisha majina baada ya Meinhof,
walifuatisha mtindo wa Meinhof, isipokuwa wanayaweka katika ngeli moja majina
ya umoja na uwingi ambayo yanachangia mzizi mmoja badala ya kuyaona kuwa ni
tofauti. Kwa uainishaji huu walipunguza idadi ya ngeli hadi kufikia 9 tu.
|
Ngeli
|
Mifano
ya Majina
|
|
1-Mu/Wa
|
Mtoto
– watoto
Mpishi
– wapishi
Mchungaji
– wachungaji
Mkulima
– wakulima
Mtu
– watu
|
|
2-
M/Mi
|
Mti
– miti
Mwembe
– miembe
Mkono
– mikono
Mchoro
– michoro
|
|
3-
Ki/Vi
|
Kiti
– viti
Kitabu-
vitabu
Kito-vito
Kisu-visu
|
|
4-
N
|
Ngozi,
nyota, nyundo, njia, ngoma, njuga
|
|
5-
Ji/Ma
|
Jiwe
– mawe
Jino
– meno
|
|
6-
U/N
|
Uzi
– nyuzi
Uso
– nyuso
Ulimi
– ndimi
Ufa
– nyufa
|
|
7-U/Ma
|
Ugonjwa
– magonjwa
Uasi
– maasi
Ununuzi
– manunuzi
|
|
8-
Ku
|
Kuimba,
kucheza, kuoga, kupiga, kusoma, kuruka, kulima
|
|
9-
KU
PA
Mu
|
Mahali
Kule
Pale
Mule
|
Uainishaji wa akina
Ashton na Broomfield unafanana na ule wa Meinfoh kwa sababu wote wameegemea
uainishaji wao katika umbo la viambishi awali vya majina. Hata hivyo uainishaji
wao umekuwa mwepesi zaidi kwa mtu anayejifunza ngeli za majina kwa vile
unaonesha uhusiano wa umbo la umoja na uwingi la majina ya aina moja. Zaidi ya
hayo uchache wa ngeli hizi unamfanya mwanafunzi azikumbuke kwa urahisi.
Matatizo
(Mapungufu) ya kigezo hiki
-
Kuna viambishi ambavyo vinafanana,
mfano, ngeli ya kwanza inawakilishwa na kiambishi Mu, kiambishi hiki kinajitokeza vilevile katika ngeli ya pili na
ngeli ya tisa. Hali kadhalika vile vya ngeli ya nne na sita vinawakilishwa na
kiambishi N-, ngeli za sita na saba
inawakilishwa na kiambishi U-. kwa
ujumla hili ni tatizo.
-
Kuna majina mengine hayana umbo dhahiri
la umoja na uwingi mfano tunda, nguo. Hivyo inakuwa vigumu kuainisha majina
yasiyo na umbo dhahiri la umoja na uwingi kwa kutumia kigezo hiki.
-
Pia kigezo hiki kinachanganya majina ya
viumbe hai na visivyo viumbe hai mfano ngeli ya tatu Ki – Vi umoja uwingi
kiti viti (kiumbe kisicho na uhai) kijana vijana (kiumbe hai)
-
Kuna baadhi ya ngeli zina viambishi vya
umoja tu mfano ngeli ya nne inatumia kiambishi cha umoja N- .
-
Pia kigezo hiki hakitilii maanani muundo
wa sentensi.
Mgullu (1999: 156) naye
amejaribu kuainisha kwa kutumia kigezo hiki cha kimofolojia. Mgullu katika
kuhitimisha uainishaji wake anasema kuwa ngeli nomino za kimofolojia katika
lugha ya Kiswahili zipo tisa yaani ngeli za:
i.
MU-WA
ii.
M-MI
iii.
JI-MA
iv.
KI-VI
v.
U-N
vi.
U-MA
vii.
U-ϴ
viii.
ϴ-MA
ix.
ZISIZO NA KIAMBISHI (CHA IDADI) CHOCHOTE
Mgullu anaendelea
kufafanua kuwa katika uainishaji huu utagundua ya kuwa nomino zilizo na umoja
na wingi tumeweziweka katika kundi moja tu. Utaona ya kuwa uainishaji huu
unatuwezesha kuzigawa nomino zote za Kiswahili bila kuibakisha hata nomino
moja. Unaweza kufikiria nomino yoyote na utapata mahali muafaka unapoweza
kuiweka.
Dosari
za uainishaji wa Mgullu ni kuwa bado matatizo tulioyataja hapo juu kwa
wataalamu na wanaisimu wengine bado hata kwa Mgullu yamejitokeza sana mfano
kufanana kwa viambishi, baadhi ya ngeli hazina umoja na wingi, pia amechanganya
majina ya viumbe hai na visivyo hai na katika uainishaji wa Mgullu hatujaona
ngeli ya PA-MU-KU.
Hitimisho
Kwa kuwa tumeshaona mapungufu na matatizo ya
uainishaji wa wataalamu na wanaisimu hao, kuna haja ya wanaisimu na wanazuoni
kuendelea kufanya utafiti na uchunguzi ili kuondoa haya mapungufu.
VITABU
VYA REJEA
Massamba, D.P.B. na
Wenzake (1999). Sarufi Miundo ya
Kiswahili Sanifu (SAMIKISA) Sekondari
na Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu, Fonetiki, Fonolojia na
Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.
Rubanza, Y.I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Dar es Salaam:
Chuo Kikuu cha Tanzania.
Taasisi ya Elimu
(1996). Kiswahili Kidato 1-4. Dar es
Salaam: Oxford University Press.
TUKI. (1981). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es
Salaam: TUKI.
Swalo, D.B. (Muswada).
Darasa la Kiswahili: Kidato cha Tano na Sita
Jumamosi, 19 Desemba 2015
Upungufu wa nguvu za kiume
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha mwisho cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.
Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Soma zaidi kuhusu mazoezi hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;
Mke wako hupendelea ukawie ikibidi ukawie zaidi. Kama mwanaume atakuwa anawahi kumaliza, basi anakuwa hampi raha mke wake.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.
Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili.
Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu la swali hili ili atakapoona tatizo ajuwe wapi pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama wanavyodhani watu wengi.
Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.
Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri unywe maji bila kusubiri kiu.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu ulio katika afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili hii ikijumuisha pia damu ya kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kuwa hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Hebu mwangalie mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna, bonyeza hapa => Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko/Stress.
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.
Katika kilele cha mwisho cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.
Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake
Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Soma zaidi kuhusu mazoezi hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;
- Umri wa mgonjwa
- Jumla ya afya aliyonayo kwa kwa sasa
- Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
- Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k
- Ni nini malengo ya tiba ?
Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii yaweza kumuacha mwanamke akiwa hakutosheka.Mke wako hupendelea ukawie ikibidi ukawie zaidi. Kama mwanaume atakuwa anawahi kumaliza, basi anakuwa hampi raha mke wake.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.
Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili.
Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
- Wasiwasi
- Hofu
- Msongo/Stress
- Hasira
- Huzuni
- Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa
- Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
- Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
- Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
- Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
- Umri mkubwa zaidi
- Kisukari
- Kujichua/Punyeto
- Uzinzi
- Kukosa Elimu ya vyakula
- Kutokujishughulisha na mazoezi
- Shinikizo la juu la damu
- Maradhi ya moyo
- Uvutaji sigara/tumbaku
- Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
- Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
- Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
- Kiwango kidogo cha homoni ya testerone
- Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Nini kinachofanya uume usimame? Kwa haraka unaweza kusema ni msisimko. Ndiyo, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha kutokea kwa msisimko huo. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu la swali hili ili atakapoona tatizo ajuwe wapi pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama wanavyodhani watu wengi.
Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.
Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri unywe maji bila kusubiri kiu.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu ulio katika afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili hii ikijumuisha pia damu ya kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kuwa hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Hebu mwangalie mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.
Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna, bonyeza hapa => Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko/Stress.
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)