Jumatano, 12 Februari 2014

Asili ya kiswahili.
kuna nadharia mbalimbali zinazoeleza kuhusu asili ya kiswahili kama vile.
(a) asili ya kiswahili ni kongo
(b) asili ya kiswahili ni pijini na krioli
(c) asili ya kiswahili ni kiarabu
(d) asili ya kiswahili ni kibantu hii ndio nadharia iliyokubaliwa na wataalam wengi kutokana na kuwepo na ushaidi wa kisayansi na kihistoria.

Nadharia zinazoeleza kuhusu chimbuko la kiswahili.
Chimbuko ni mahali pale ambapo kitu kimeazia. Zifuatazo na nadharia zinazo eleza kuhusu chimbuko la kiswahili, nazo ni
(a) chimbuko la kiswahili ni kongo
(b) chimbuko la kiswahili ni kameruni
(c) chimbuko la kiswahili ni pwani ya Afrika mashariki; hii ndio nadharia inayothibitisha kuhusu chimbuko la kiswahili kutokana na ushaidi ufuatao
(i) mgawanyo wa lajaha huko pwani ya afrika mashariki.
(ii) hata lahaja ya usanifishaji ilitoka pwani ya afrika mashariki nayo ni kiunguja.
(iii) wazangumzaji wengi wa kiswahili wako pwani ya afrika mashariki
(iv) hata wengeni wa kwanza kufika afrika mashariki walikuta wenyeji wa mwambao wanazungumza kiswahili.