Jumatano, 1 Juni 2016

UHUSIANO BAINA YA UNYAMBULISHAJI NA SINTAKSIA



Mchakato wowote unapofanyika huleta athari fulani kwenye tungo au neno linalohusika. Unyambulishaji ni moja ya mchakato ambao ukifanyika katika kitenzi unaleta athari katika vitenzi hivyo.        

 Na mchakato huu unaonesha uhusiano uliopo baina ya sintaksia na vitenzi vinavyonyambulishwa na visivyonyambulishwa. Hivyo, kuna baadhi ya vitenzi vikinyambulishwa vinachukua dhima moja na vingine vinachukua dhima mbili. Na kuna vitenzi  kwa asili yake havihitaji yambwa lakini unyambulishaji unavifanya vitenzi hivyo kuwa na sulubu dhima.   
          Uhusiano baina ya unyambulishaji na sintaksia unajitokeza katika mambo makuu matatu, kama ifuatavyo:
Kuongeza dhima                                                                                                                                Uongezaji dhima, utokea pale ambapo kitenzi ambacho hakina uwezo wa kubeba yambwa, hunyumbulishwa na kulazimishwa kubeba yambwa. Mchakato wa unyambulishi unakiwezesha kitenzi chenye sulubu dhima ya msingi kushiriki katika sulubu dhima nyingine na kwa kufanya hivyo huwezesha sentensi mbili kutungwa. Mfano:                                                                      
Ali amekufa (sulubu dhima moja)                                                                               tk
Ali amelif-i-a taifa lake (sulubu dhima mbili)                                                      td                                 tk
Katika mchakato huu wa kuongeza dhima au uongezaji dhima, kuna aina mbili za unyambulishaji zinazojitokeza nazo ni: unyambulishaji mufidi na unyambulishaji fanyizi.                            Unyambulishaji mufidi huu ni unyambulishaji wa uongezaji dhima kwa njia ya kupachika alomofo za kauli ya utendea yaani –e- na –i- katika kitenzi. Mfano:
       Swalo anapika (sulubu dhima moja)                                                                                                               tk        
        Swalo anampik-i-a mtoto (sulubu dhima mbili)                                                                                  td                    +fd    tk
       Stivin anasoma (sulubu dhima moja)                                                                                                           td
     Stivin anamsom-e-a Musa kitabu (sulubu dhima tatu)                                                                                       td                  +fd                 
           
Unyambulishi fanyizi, ni unyambulishi wa uongezaji dhima unaohusu upachikaji wa alomofu za kauli ya utendeshi katika kitenzi, alomofu hizo ni; -esh-, -ish-, na –z-. Mfano:
  Mtoto anaimba (sulubu dhima moja)                                                                                                  mtenda
 Mtoto anaimb-ish-a wimbo (sulubu dhima mbili)                                                                               mtenda                                    tk
Kupunguza dhima, uhusiano wa unyambulishi na sintaksia, pia hujidhihirisha katika upunguzaji dhima. Mchakato huu husababisha kauli tenda kubadilika na kuwa kauli tendeka baada ya kupachika alomofu za kauli ya kutendeka –k-, -ik- na –ek- na hivyo kitenzi chenye dhima ya utenda kupoteza dhima hiyo kutokana na unyambulishi tendeka. Mfano:
          Ali amemshik-i-a mwalimu kitabu (sulubu dhima tatu)                                                                      td                                 tk         tu
          Ali amekishik-il-a kitabu (sulubu dhima mbili)                                                                                   td                              tk
Hivyo, kitendo cha kubadili kauli tenda kwenda kauli tendeka kunachangia kuleta athari kubwa katika sintaksia kwani hupunguza dhima ya kitenzi katika sentensi.                                                            
   Kudhibiti dhima, hapa mchakato wa unyambulishi unapewa dhima mpya bila kubadili idadi ya dhima ndani ya sulubu dhima. Matokeo ya mchakato huu ni kwamba, kitenzi kinachatokea katika sulubu dhima na idadi ile ile ya nomino lakini dhima tofauti. Hapa kitenzi kipya hupata kauli tendwa na kuambikwa umbo la –w-. Mfano:
                   Swalo anapika chakula                                                                                   
                  Chakula kinapikwa na Swalo                                                                                                             
Mifano hiyo hapo juu, inaonesha kuwa sulubu dhima ni ileile, idadi  ya nomimo ni ileile, lakini tofauti ni ubadilishananji wa nafasi kati ya kiima na yambwa yaani sentensi ya pili, nafasi ya kiima imechukuliwa na yambwa na nafasi ya yambwa imechukuliwa na kiima.

Ijumaa, 29 Januari 2016

KAMATA FURSA AMBAYO HAITAKUPOTEZEA MUDA



KAMATA FURSA AMBAYO HAITAKUPOTEZEA MUDA
RIFARO AFRICA          ni kampuni mama kutoka Tanzania yenye lengo la kumsaidia mmiliki wa simu ya mkononi kuweza kunufaika na muda wa hewani anaoutumia kwa kumuingizia kipato.                                                                                                       Kampuni hili ilipata wazo hili toka mwaka 2011, lakini rasmi ilianza kulifanyia kazi mwaka 2014 mara baada ya taasisi zote muhimu kuipitia na kujiridhisha na utendaji utakaoenda kumsaidia mtumiaji wa simu kwamba uko sahihi.
BIDHAA                                                                                                               Kampuni imetuletea bidhaa makini sana, muda wa hewani yaani AIRTIME bidhaa ambayo katika hali ya sasa hivi ina umuhimu mkubwa sana, iwe ni mchana  au usiku, wakati wa shida ama raha bado tunaitumia sana. KUMBUKA SIMAANISHI KUA UNAKUWA MUUZA VOCHA BALI KWA MATUMIZI YAKO BINAFSI NA UNALIPWA.

MFUMO                                                                                                                    Rifaro Africa inaendesha biashara katika mfumo wa mtandao yaani Network marketing. Biashara ya karne ya 21, biashara ambayo inakufanya uachane na kutumia nguvu nyingi, biashara ambayo itakupatia kipato ambacho hakina kikomo, uwepo usiwepo biashara yako huendelea kuwepo.                                                                 Rifaro wameuweka mfumo huu katika vizazi 15. Utalipwa kuanzia kizazi cha 1-15   kwa uwiano tofauti kulingana na kizazi kwa kizazi.  
AINA ZA MALIPO
Malipo ya wiki                                                                                                             Haya ni malipo yanayotokana na kazi uliyoifanya wewe kwa kushirikiana na washirika wako katika biashara kuanzia kizazi cha kwanza hadi kumi na tano.
MALIPO YAPO HIVI                                                                                                 Kizazi 1: 20000/= kwa kila atakayeingia kwako moja kwa moja                                     Kizazi 2: 8000/=                                                                                                        Kizazi 3: 5000/=                                                                                                       Kizazi 4: 5000/=                                                                                                        Kizazi 5: 5000/=                                                                                                        Kizazi 6: 3000/=
Kizazi cha 7 hadi 15 utalipwa 2000 kwa kila kizazi.
Mfano kwa mwezi ukaingiza watu 10 na kila mtu kati ya hao 10 akaingiza watu 10 inaweza kuwa hivi.
1)     20000x10= 200000
2)     8000x100=800000
3)     5000x10000= 5m
4)     5000x10000= 50m
5)     5000x100000= ni zaidi ya 500m
MTAJI                                                                                                                        Kama zilivyo biashara nyingine, hii pia itakuhitaji uwekeze mtaji wa 128, 500 na utapatiwa DVD, ATM card (yenye 2000 ndani yake), kitabu cha biashara,website (kukuwezesha kuingia kwenye ofisi yako, kuona biashara yako yote) salio vocha 5000 na namba ya mwanachama.
Kwanini mtu anahitaji kujiunga na kampuni ya rifaroafrica?
·        Unalipwa fedha kwa miaka yote na hata baada ya muda wako wa kuishi.
·        Rifaro ina hadhi kubwa kwa sababu imeaminiwa na hata kufanya kazi kwa kushirikiana na makampuni ya simu nchini, yanayomiliki uchumi  wa Tanzania.
·        Inafanya kazi na selcom, kampuni kubwa duniani.
·        Rifaro inatumia ATM visa card yake wakati yenyewe sio benki.
·        Rifaro ina ofisi kila mkoa, kila wilaya nchi nzima.
·        Rifaro ni halali, imesajiliwa kisheria na mamlaka zote, TCRA, BRELA na TRA.
·        Rifaro in mawakala wa selcom machines kila kona ya nchi ya Tanzania.
·        Rifaro ni pekee kukufanya ulipwe kwa kutumia simu yako kutatua matatizo yako mwenyewe.


Una hofu gani? Unasubiri nini? Jiunge sasa na rifaro, urithi pekee kwa mwanao na vizazi vyako maana ajira yako, biashara yako na cheo chako havirithishwi ng’o line zako na biashara yako ya rifaro inarithishwa.
Karibu ujiunge kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na mimi DICKSON SWALO kupitia
0752642389 au 0673642389

Jumanne, 19 Januari 2016

Ngeli za nomino za kiswahili




SWALI: Kwa kutumia mifano, ainisha ngeli za nomino za Kiswahili, kwa kigezo cha kimofolojia. Kisha jadili upungufu wa uainishaji huo.
                                               
                                                               
Fasili ya ngeli imejadiliwa na wataalamu na wanazuoni mbalimbali, huku kila mtaalamu akiwa na mtazamo wake juu ya dhana hii. Baadhi ya wataalamu na wanazuoni hao ni kama hawa wafuatayo:
Mgullu (1999: 148) anasema istilahi “ngeli” imechukuliwa kutoka lugha ya Kihaya (Tanzania). Katika lugha ya kihaya neno “ngeli” lina maana ya aina ya kitu. 

Mgullu (1999: 148) akiinukuu Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981) anaeleza kuwa ngeli ni utaratibu wa taaluma ya sarufi ya lugha katika kupanga aina za majina (nomimo) kama vile ki-vi, ma, n.k.
Mgullu anaendelea kusema kuwa fasili hii inapotosha. Tuaamini ya kuwa ngeli ni kundi la nomino za aina moja na si ule utaratibu wa kupanga nomino katika makundi kama fasili ya hapo juu inavyodai.
TUKI (1990) wanaeleza kuwa ngeli za nomino ni kundi moja la majina yaliyo na upatanisho wa kisarufi unaofanana na viambishi vya umoja na wingi vinavyofanana. Fasili hii inaonekana ni bora lakini tatizo lake ni kuwa imeweka pamoja vigezo viwili, yaani kigezo cha kisintaksia na kile cha kimofolojia. Kwa maoni yangu ni kuwa vigezo hivi haviwezi kutumika pamoja kwa sababu havina uhusiano wa moja kwa moja. Wanaisimu na wachambuzi wengi wa awali walijaribu kuvitumia vigezo vyote viwili kwa pamoja wakati wa kuainisha ngeli za nomino za Kiswahili lakini walishindwa. Hali hii imesababisha uainishaji wa ngeli katika lugha ya Kiswahili uonekane kuwa wa kutatanisha.

Massamba, D.P.B na Wenzake (2012) wanasema kauli kwamba ngeli ni mgawanyiko wa aina mbalimbali za nomino katika mtazamo wa kisarufi katika fikra ya viashirio vya nomino katika aina nyingine za maneno zinazoandamana nazo. Kwa maelezo mafupi tunaweza kusema ngeli za nomino huhusu makundi ya majina; kila kundi likiwa na mabadiliko ya aina moja ya viambishi vya umoja na wingi vyenye kuleta upatanishi wa kisarufi wa namna moja katika vitenzi, vivumishi na viwakilishi. Kila ngeli ina kiambishi cha nomino zake ambacho kinatawala viambishi vinavyorejea nomino hiyo katika aina hizo nyingine ziandamanazo nayo.

Massamba na Wenzake wanaendelea kufafanua kuwa kila lugha inayotumia utaratibu wa ngeli huwa ina idadi fulani ya ngeli. Si rahisi kusema kwa yakini hapo zamani lugha za kibantu zilikuwa na ngeli ngapi, lakini tunajua kwamba kwa wastani lugha nyingi zina ngeli zisizopungua kumi na zisizozidi ishirini. 

Kwa ujumla, ngeli ni aina au namna ya kupanga au kuweka majina katika makundi yanayofanana au yanayowiana. Majina ya Kiswahili yanaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali. Baadhi ya wanaisimu wamegawanya majina katika makundi 16 na wengine katika makundi 9 na wengine makundi 18. Wanaisimu tofauti walioainisha ngeli za majina ya Kiswahili wamechunguza vipengele tofauti  vya majina na kuyaanisha tofauti. Nomino za lugha fulani zinaweza kuainishwa kwa kutumia vigezo vikuu vitatu yaani:
·        
            Kigezo cha kisematiki
·         Kigezo cha kimofolojia
·         Kigezo cha kisintaksia

Lakini katika muktadha huu tutajikita katika kujadili uainishaji wa ngeli za Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kimofolojia. Kigezo cha kimofolojia ni kigezo kikongwe zaidi kilichotumiwa na wanasarufi mapokeo, miongoni mwao akiwa Meinhof ambao waliyaainisha kulingana na maumbo ya viambishi awali vya majina. Majina yote yalikuwa na viambishi awali vinavyofanana yaliwekwa katika kundi moja na kufanya ngeli moja kutokana na kigezo hiki kuna ngeli 18 za Kiswahili. Uainishaji wao ni kama ifuatavyo:
Ngeli
Mfano wa majina ya Ngeli
1-Mu-
2-Wa-
Mzee – wazee
Mtoto- watoto
3- M-
4- Mi-
Mti – miti
Mchungwa – michungwa
5- Ki-
6- Vi-
Kiti- viti
Kisu- visu
7- Ji-
8- Ma-
Jiwe- mawe
Jicho- macho
9- N-
10.
Nguo, nchi, njaa, nyota, ngozi, nyama
11- U-
12- N-
Uso – nyuso
Uzi – nyuzi
Ulimi- ndimi
13- U-
14- Ma-
Uasi – maasi
Ugonjwa – magonjwa
15- Ku-
Kusoma
Kucheza
Kuimba
Kuruka
16- Pa-
Pahali
17- Mu-
Muhali
18- Ku-
Kuhali

Wanaisimu wengine Ashtoni (1944) na Broomfield (1930) waliainisha majina baada ya Meinhof, walifuatisha mtindo wa Meinhof, isipokuwa wanayaweka katika ngeli moja majina ya umoja na uwingi ambayo yanachangia mzizi mmoja badala ya kuyaona kuwa ni tofauti. Kwa uainishaji huu walipunguza idadi ya ngeli  hadi kufikia 9 tu.
Ngeli
Mifano ya Majina
1-Mu/Wa
Mtoto – watoto
Mpishi – wapishi
Mchungaji – wachungaji
Mkulima – wakulima
Mtu – watu
2- M/Mi
Mti – miti
Mwembe – miembe
Mkono – mikono
Mchoro – michoro
3- Ki/Vi
Kiti – viti
Kitabu- vitabu
Kito-vito
Kisu-visu
4- N
Ngozi, nyota, nyundo, njia, ngoma, njuga
5- Ji/Ma
Jiwe – mawe
Jino – meno
6- U/N
Uzi – nyuzi
Uso – nyuso
Ulimi – ndimi
Ufa – nyufa
7-U/Ma
Ugonjwa – magonjwa
Uasi – maasi
Ununuzi – manunuzi
8- Ku

Kuimba, kucheza, kuoga, kupiga, kusoma, kuruka, kulima

9- KU
    PA
    Mu
Mahali Kule
            Pale
            Mule

Uainishaji wa akina Ashton na Broomfield unafanana na ule wa Meinfoh kwa sababu wote wameegemea uainishaji wao katika umbo la viambishi awali vya majina. Hata hivyo uainishaji wao umekuwa mwepesi zaidi kwa mtu anayejifunza ngeli za majina kwa vile unaonesha uhusiano wa umbo la umoja na uwingi la majina ya aina moja. Zaidi ya hayo uchache wa ngeli hizi unamfanya mwanafunzi azikumbuke kwa urahisi.

Matatizo (Mapungufu) ya kigezo hiki
-          Kuna viambishi ambavyo vinafanana, mfano, ngeli ya kwanza inawakilishwa na kiambishi Mu, kiambishi hiki kinajitokeza vilevile katika ngeli ya pili na ngeli ya tisa. Hali kadhalika vile vya ngeli ya nne na sita vinawakilishwa na kiambishi N-, ngeli za sita na saba inawakilishwa na kiambishi U-. kwa ujumla hili ni tatizo.
-          Kuna majina mengine hayana umbo dhahiri la umoja na uwingi mfano tunda, nguo. Hivyo inakuwa vigumu kuainisha majina yasiyo na umbo dhahiri la umoja na uwingi kwa kutumia kigezo hiki.  
-          Pia kigezo hiki kinachanganya majina ya viumbe hai na visivyo viumbe hai mfano ngeli ya tatu Ki – Vi                                                                                                                                                              umoja           uwingi                                                                                                                              kiti                 viti   (kiumbe kisicho na uhai)                                                                                      kijana               vijana (kiumbe hai) 
-          Kuna baadhi ya ngeli zina viambishi vya umoja tu mfano ngeli ya nne inatumia kiambishi cha umoja N- .
-          Pia kigezo hiki hakitilii maanani muundo wa sentensi.

Mgullu (1999: 156) naye amejaribu kuainisha kwa kutumia kigezo hiki cha kimofolojia. Mgullu katika kuhitimisha uainishaji wake anasema kuwa ngeli nomino za kimofolojia katika lugha ya Kiswahili zipo tisa yaani ngeli za:
          i.            MU-WA
        ii.            M-MI
      iii.            JI-MA
      iv.            KI-VI
        v.            U-N
      vi.            U-MA
    vii.            U-ϴ
  viii.            ϴ-MA
      ix.            ZISIZO NA KIAMBISHI (CHA IDADI) CHOCHOTE

Mgullu anaendelea kufafanua kuwa katika uainishaji huu utagundua ya kuwa nomino zilizo na umoja na wingi tumeweziweka katika kundi moja tu. Utaona ya kuwa uainishaji huu unatuwezesha kuzigawa nomino zote za Kiswahili bila kuibakisha hata nomino moja. Unaweza kufikiria nomino yoyote na utapata mahali muafaka unapoweza kuiweka.                                               

    Dosari za uainishaji wa Mgullu ni kuwa bado matatizo tulioyataja hapo juu kwa wataalamu na wanaisimu wengine bado hata kwa Mgullu yamejitokeza sana mfano kufanana kwa viambishi, baadhi ya ngeli hazina umoja na wingi, pia amechanganya majina ya viumbe hai na visivyo hai na katika uainishaji wa Mgullu hatujaona ngeli ya PA-MU-KU.

Hitimisho                                                                                                                                             Kwa kuwa tumeshaona mapungufu na matatizo ya uainishaji wa wataalamu na wanaisimu hao, kuna haja ya wanaisimu na wanazuoni kuendelea kufanya utafiti na uchunguzi ili kuondoa haya mapungufu.



                                            VITABU VYA REJEA   
Massamba, D.P.B. na Wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA) Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.

Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa Isimu, Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi: Longhorn Publishers.

Rubanza, Y.I. (1996). Mofolojia ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Tanzania.

Taasisi ya Elimu (1996). Kiswahili Kidato 1-4. Dar es Salaam: Oxford University Press.

TUKI. (1981). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.

Swalo, D.B. (Muswada). Darasa la Kiswahili: Kidato cha Tano na Sita