Mchakato
wowote unapofanyika huleta athari fulani kwenye tungo au neno linalohusika.
Unyambulishaji ni moja ya mchakato ambao ukifanyika katika kitenzi unaleta
athari katika vitenzi hivyo.
Na
mchakato huu unaonesha uhusiano uliopo baina ya sintaksia na vitenzi
vinavyonyambulishwa na visivyonyambulishwa. Hivyo, kuna baadhi ya vitenzi
vikinyambulishwa vinachukua dhima moja na vingine vinachukua dhima mbili. Na
kuna vitenzi kwa asili yake havihitaji
yambwa lakini unyambulishaji unavifanya vitenzi hivyo kuwa na sulubu dhima.
Uhusiano
baina ya unyambulishaji na sintaksia unajitokeza katika mambo makuu matatu,
kama ifuatavyo:
Kuongeza dhima Uongezaji dhima, utokea
pale ambapo kitenzi ambacho hakina uwezo wa kubeba yambwa, hunyumbulishwa na
kulazimishwa kubeba yambwa. Mchakato wa unyambulishi unakiwezesha kitenzi
chenye sulubu dhima ya msingi kushiriki katika sulubu dhima nyingine na kwa
kufanya hivyo huwezesha sentensi mbili kutungwa. Mfano:
Ali amekufa (sulubu
dhima moja) tk
Ali amelif-i-a taifa
lake (sulubu dhima mbili) td tk
Katika
mchakato huu wa kuongeza dhima au uongezaji dhima, kuna aina mbili za
unyambulishaji zinazojitokeza nazo ni: unyambulishaji mufidi na unyambulishaji
fanyizi. Unyambulishaji
mufidi huu ni unyambulishaji wa uongezaji dhima kwa njia ya kupachika alomofo
za kauli ya utendea yaani –e- na –i- katika kitenzi. Mfano:
Swalo
anapika (sulubu dhima moja) tk
Swalo
anampik-i-a mtoto (sulubu dhima mbili) td +fd tk
Stivin
anasoma (sulubu dhima moja) td
Stivin
anamsom-e-a Musa kitabu (sulubu dhima tatu) td +fd
Unyambulishi
fanyizi, ni unyambulishi wa uongezaji dhima unaohusu upachikaji wa alomofu za
kauli ya utendeshi katika kitenzi, alomofu hizo ni; -esh-, -ish-, na –z-.
Mfano:
Mtoto anaimba
(sulubu dhima moja) mtenda
Mtoto
anaimb-ish-a wimbo (sulubu dhima mbili) mtenda tk
Kupunguza
dhima, uhusiano wa unyambulishi na sintaksia, pia hujidhihirisha katika
upunguzaji dhima. Mchakato huu husababisha kauli tenda kubadilika na kuwa kauli
tendeka baada ya kupachika alomofu za kauli ya kutendeka –k-, -ik- na –ek- na
hivyo kitenzi chenye dhima ya utenda kupoteza dhima hiyo kutokana na
unyambulishi tendeka. Mfano:
Ali
amemshik-i-a mwalimu kitabu (sulubu dhima tatu) td tk tu
Ali
amekishik-il-a kitabu (sulubu dhima mbili) td tk
Hivyo,
kitendo cha kubadili kauli tenda kwenda kauli tendeka kunachangia kuleta athari
kubwa katika sintaksia kwani hupunguza dhima ya kitenzi katika sentensi.
Kudhibiti
dhima, hapa mchakato wa unyambulishi unapewa dhima mpya bila kubadili idadi ya
dhima ndani ya sulubu dhima. Matokeo ya mchakato huu ni kwamba, kitenzi kinachatokea
katika sulubu dhima na idadi ile ile ya nomino lakini dhima tofauti. Hapa
kitenzi kipya hupata kauli tendwa na kuambikwa umbo la –w-. Mfano:
Swalo
anapika chakula
Chakula
kinapikwa na Swalo
Mifano
hiyo hapo juu, inaonesha kuwa sulubu dhima ni ileile, idadi ya nomimo ni ileile, lakini tofauti ni
ubadilishananji wa nafasi kati ya kiima na yambwa yaani sentensi ya pili,
nafasi ya kiima imechukuliwa na yambwa na nafasi ya yambwa imechukuliwa na
kiima.