Jumamosi, 19 Desemba 2015

Upungufu wa nguvu za kiume

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha mwisho cha furaha katika maisha ya ndoa, kama inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.
Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.
Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala pengine; zinatoka katika vyakula tu.

Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake

Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?

Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni.
Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri. Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo, wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Soma zaidi kuhusu mazoezi hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu, magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume. Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;
  • Umri wa mgonjwa
  • Jumla ya afya aliyonayo kwa kwa sasa
  • Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
  • Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k
  • Ni nini malengo ya tiba ?
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako, kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya tatizo linalokukabili.

Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?

Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa raha (orgasm), hali hii yaweza kumuacha mwanamke akiwa hakutosheka.
Mke wako hupendelea ukawie ikibidi ukawie zaidi. Kama mwanaume atakuwa anawahi kumaliza, basi anakuwa hampi raha mke wake.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako. Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili. Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.
Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili.
Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya mhemko kama;
  • Wasiwasi
  • Hofu
  • Msongo/Stress
  • Hasira
  • Huzuni
  • Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa
Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
  1. Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
  2. Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
  3. Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
  4. Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea pia kama kipengele kimojawapo katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo sawa. Pia sababu zingine za kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au kuwahi kufika kileleni ni pamoja na;
  • Umri mkubwa zaidi
  • Kisukari
  • Kujichua/Punyeto
  • Uzinzi
  • Kukosa Elimu ya vyakula
  • Kutokujishughulisha na mazoezi
  • Shinikizo la juu la damu
  • Maradhi ya moyo
  • Uvutaji sigara/tumbaku
  • Utumiaji uliozidi wa kafeina. Na kama hujuwi kafeina ni kitu gani, bonyeza => hapa.
  • Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
  • Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
  • Kiwango kidogo cha homoni ya testerone
  • Athari kutoka kwa baadhi ya dawa

Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:

Nini kinachofanya uume usimame? Kwa haraka unaweza kusema ni msisimko. Ndiyo, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha kutokea kwa msisimko huo. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu la swali hili ili atakapoona tatizo ajuwe wapi pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani, Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama wanavyodhani watu wengi.
Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo kujidhuru badala ya kujitibu.
Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri unywe maji bila kusubiri kiu.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.
Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].

Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu ulio katika afya bora husambaza damu ya kutosha katika viungo vyote vya mwili hii ikijumuisha pia damu ya kwenye mishipa ya uume wako. Hii ni kuwa hata kama utagusana na mwanamke hautaweza kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako kama inavyotakiwa. Hebu mwangalie mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60 kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda mwenyewe.

Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume

Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!.
Utajuwaje kama una msongo wa mawazo au stress? ili kujuwa kama una stress au hauna, bonyeza hapa => Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko/Stress.
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli, kisukari, shinikizo la damu na hata uzito ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni